1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtafaruku na mauwaji mjini Prt-Au-Prince

28 Februari 2004

PORT-AU-PRINCE: Hali ya fujo, machafuko na mauwaji imezidi kuongezeka katika mji mkuu wa Haiti unaozingirwa na waasi. Ubalozi wa Marekani umesema kwa sehemu hali hiyo imesababishwa na wafuasi wa Rais Jean Bertrand Aristide. Wanajeshi wa serikali wameezeka vizuizi vya njiani na kuvitia moto katikati ya mji mkuu, kufanya wizi wa maduka na kuuawa watu. Shirika la Utangazaji la Kimarekani CNN limeripoti kuwa watu kadha wamejinchwa kikatili njiani. Mkuu wa waasi Guy Philippe ametangaza kwamba kabla ya kuanzisha operesheni ya kuuvamia mji mkuu, kwanza anauzingira kwa sababu ni vigumu kuuteka. Katika tangazo la televisheni Rais Aristide amekataa kujiuzulu kabla ya kumalizika muda wa utawala wake hapo 2006. Jamhuri jirani ya Dominican imeanza kuwahamisha wageni kwa njia ya helikopta kutoka Haiti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW