Mtambue hayati Bi Kidude
18 Aprili 2013Yeyote akimuuliza kuhusu umri wake wake anasema hawezi kuutaja lakini alizaliwa zama za sarafu ya rupia. Ilikuwa sarafu iliyotumiwa katika eneo la Afrika Mashariki mpaka wakati wa vita vya kwanza vya dunia. Bi Kidude si kwamba alikuwa na mvuto kwa sauti yake nzuri ya kuimba taarab lakini pia namna ya muonekano wake katika jukwaa. Ingawa alikuwa mzee lakini alikuwa maarufu na mwenye kufurahisha watu wa umri tofauti hadi vijana.
Taarab ni mchanganyiko wa musiki wa Kiarabu na kiafrika
Taarabu ni sehemu ya mchanganyiko wa muziki wa Kiswahili na wenye kuchanganyika na Kihindi na Kiarabu inatumia ala za udi, fidla, filimbi na ngoma. Kwa kiasi kikubwa muingiliano wa tamaduni za Kiswahili na Kiarabu unatokana Zanzibar kuwa mji wa uliyochini ya mamlaka ya Sultan wa Oman. Zanzibar ilikuwa kituo cha biashara ya utumwa kwa mataifa ya rasi ya kiarabu.
1920, Bi Kidude alikuwa akiimba rasmi katika matamasha ya kitamadauni. Alizaliwa katika kijiji kidoko Mfagimalingo mjini Unguja, alikuwa ni mwimbaji wa kwanza wa kike katika eneo la Zanzibar. Ilikuwa ni hatua kubwa kwa wanawake hasa wanawake wanaovaa baibui vazi la kujisitiri kwa wanawake wa Pwani ya afrika mashariki.
Kupigania haki za wanawake
Alikuwa na ujasiri mkubwa wakati alipotoroka katika visiwa vya Zanzibar kukwepa ndoa ya lazima akiwa na umri wa miaka 13. Baadae akawa mtu anaejihusisha sana na muziki wa taarab kwa kufanya ziara mbalimbali za muziki huo katika maeneo ya afrika mashariki.
Baada ya kurejea Zanzibar 1940, pamoja na kuwa mtu mwenye umaarufu mkubwa lakini aliendelea kuishi katika nyumba yake iliyotengenezwa kwa udongo. Mbali na muziki alikuwa akijihusisha na vyama vya kijamii na kutoa elimu ya unyago kwa wasichana katika visiwa hivyo.
Taarabu ni maisha yangu
Kwa kutumia muziki wenye hisia na huzuni Bi Kidude aliimba kwa mtindo wa aina yake wenye mvuto. Hakuweza kujali kuhusu miiko, aliolewa mara mbili, na alikuwa anavuta sigara na mwaka uliyopita akikuwa anakunywa sana pombe. Katika jamii isiyopenda mabadikilo lakini aliweza kuishi.
Wakati akiwa katika jukwaa alikuwa akipebnda kubadili miondoko. Kwa hiyo alikuwa akitoa wakati mgumu sana kwa wanamuziki wanaompogia vyombo mbalimbali katika bendi husika kwa wakati huo.
Washabiki wake walikuwa wakipenda sana mawazo yake ya kubadili miondoko au nyimbo akiwa katika jukwaa. Ingawa mwanamke huyo alikuwa mwenye umbo dogo lakini alikuwa akipiga ngoma katika kiwango cha kushangaza wengi.
Mirindimo yake na namna alivyokuwa na nguvu na uwezo wa kupiga ngoma ilikuwa ikishangaza sana idadi kubwa ya watu mpaka mwaka uliyopita. 2005 alipata tuzo kutokana na kutukuza muziki na utamaduni wa Zanzibar. Bi Kidude alikufa baada ya kuugua kwa muda mrefu katika nyumba yake ndogo mjini Zanzibar ambayo ndimo yalikuwa makazi yake. Wakazi wa visiwa vya Zanzibar na kwengineno wanaomboleza kifo cha malkia wa Taarab Bi. Kidude.
Mwandishi: Andrea Schmidt/Sudi Mnette
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman