Mtandao umeviwezesha vitongoji maskini nchini Kenya
2 Aprili 2022Katika hatua ya kwanza ya utendaji wa kampuni ya Poa Internet, inalenga kutoa huduma ya mtandao wenye gharama nafuu kwa watu wenye vipato vya chini nchini Kenya. Kazi ya Nzoma, hujumuisha "kuweka taarifa inayohusu jiografia ya eneo", ambapo unahitaji mtandao wenye kasi ya juu na unaoaminika.
Kampuni hiyo yenye mtandao wa bei nafuu, imeunganisha mtandao wake kwenye migahawa,majengo marefu na nyumba 12000 ndani ya jinji la Nairobi. Mtendaji mkuu wa Poa Internet, Andy Halsall alisema´´ tunatumia mtandao usiotumia waya ili kufiki nyumba za wateja na hii ina tupunguzia gharama,"
Kenya ni mmoja ya nchi iliyounganishwa zaidi barani Afrika ambapo asilimia 42% ya raia wa kenya wamekuwa mtandaoni mwanzoni mwa 2022, kulingana na watafiti wa mtandao . Ijapokuwa ubora wa uunganishwaji huo ni wa hadhi ya chini.
Mtandao huu wa bei nafuu na kasi ya haraka " umerahisisha upatikanaji wa kazi,biashara,elimu na ujumuishaji wa kijamii. Watu wengi huko huunganisha kupitia simu zao na hutumia vifurushi vya data vya 3G au 4G.
Soma zaidi:Serikali ya Zimbabwe yaamuru kufungwa kwa huduma za intaneti
Nzoma hulipa shilingi 2,500 za Kenya kila mwezi kwa mtandao wa kasi usio na kikomo, karibu nusu ya ada zinazotozwa na wengine watoa huduma za mtandao na nafuu zaidi kuliko bando za data za simu, zinazotolewa na makampuni kama Airtel au Safaricom.
Mnamo Januari, kampuni ya Poa ilifunga mzunguko wa ufadhili wa dola milioni 28 ulioongozwa na mfuko wa miundombinu Afrika50. Inatarajia kupanua wigo wake zaidi ya Kenya.Halsall alisema kampuni hiyo yenye miaka mitano italeta faida ndani ya mwaka mmoja.