1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMsumbiji

Mtandao wa simu za mkononi wakatwa Maputo

26 Oktoba 2024

Mawasiliano ya simu za mkononi yalikatwa jana Ijumaa katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo baada ya maandamano ya kupinga ushindi wa mgombea wa urais kupitia chama tawala Frelimo.

Gharama za intaneti nchini Msumbiji
Mmoja ya watumiaji wa simu za mkono katika mji wa Maputo nchini Msumbiji. Iliripotiwa mtandao ulikatwa baada ya maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa raisPicha: DW

Mwandishi wa habari wa AFP aliripoti tatizo hilo la kukatika kwa mtandao lakini kwa simu za mkononi tu.

Tume ya uchaguzi nchini humo siku ya Alhamisi ilimtangaza mgombea wa Frelimo Daniel Chapo kushinda uchaguzi wa urais kwa asilimia 71 ya kura zote, hatua iliyobua ghadhabu kutoka upande wa upinzani.

Kulishuhudiwa maandamano zaidi jana Ijumaa katika mji huo mkuu, baada ya yale ya Alhamisi ya wafuasi wa upinzani waliopinga kile walichoita wizi wa kura uliofanywa na tume inayopendelea chama tawala.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW