1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
TeknolojiaMarekani

Mtandao wa TikTok wazimwa Marekani

19 Januari 2025

Mtandao wa kijamii wa TikTok umesitisha huduma zake nchini Marekani kuanzia Jumamosi usiku na kufuta programu yake kwenye Google na Apple store.

Programu ya video ya Tiktok imeacha kufanya kazi Marekani
Mtandao wa kijamii wa TikTok umesitisha huduma zake nchini Marekani.Picha: Andrej Sokolow/picture alliance/dpa

Haya yamejiri kabla ya sheria itakayoanza kutumika Jumapili inayohitaji kuzimwa kwa jukwaa hilo linalotumiwa na takriban Wamarekani milioni 170.

Kwa mujibu wa chapisho lililowekwa na Tiktok, Rais mteule Donald Trump, amesema kuna "uwezekano" wa  kuahirisha kwa siku 90 marufuku hiyo mara baada ya kuchukua madaraka siku ya Jumatatu.

Soma pia: Venezuela yautoza faini ya dola milioni 10 mtandao wa TikTok

Hata ikiwa ni ya muda mfupi, kuzimwa kwa TikTok, inayomilikiwa na kampuni ya teknolojia ya China  ByteDance , kunatarajiwa kuwa na athari kubwa katika uhusiano wa Marekani na China, siasa za ndani za Marekani, kijamii soko la vyombo vya habari na mamilioni ya Wamarekani ambao wanategemea mtandao huo kiuchumi na kiutamaduni.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW