1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtanzania Abdulrazak Gurnah ashinda tuzo ya Nobel ya Fasihi

7 Oktoba 2021

Tuzo ya Nobel katika fasihi imetolewa mwaka huu kwa mwandishi wa Kitanzania Abdulrazak Gurnah, kutokana na kazi yake kuhusu athari za ukoloni na hatima ya mkimbizi.

Abdulrazak Gurnah | Gewinner Literaturnobelpreis 2021
Picha: Chapter of Canterbury Cathedral/Reuters

Nishani ya Nobel katika Fasihi kwa mwaka huu wa 2021 imetolewa kwa mwandishi wa Kitanzania Abdulrazak Gurnah, kutokana na kazi yake kuhusu athari za ukoloni na hatima ya mkimbizi, imetangaza taasisi ya Sweden siku ya Alhamisi.

Gurnah alizaliwa visiwani Zanzibar mwaka 1948, lakini kufuatia mwisho wa ukoloni wa Uingereza 1963, alikabiliwa na mateso kutokana na asili yake ya Kiarabu, na alilazimika kukimbia, na hatimaye kuwasili nchini Uingereza kama mkimbizi mwishoni mwa miaka ya 1960.

Akiishi Uingereza tangu wakati huo, alifundisha katika Chuo Kikuu cha Kent hadi kustaafu kwake.

"Tunafurahi kabisa kuwa mhadhiri wetu wa zamani Abdulrazak Gurnah amepewa Tuzo ya Nobel ya fasihi - Ni jambo la kufurahia kweli!" kiliandika chuo hicho katika ujumbe wa twitter.

Baadhi ya vitabu alivyoandika Abdulrazak Gurnah.Picha: Jonathan Nackstrand/AFP/Getty Images

Gurnah ameandika riwaya 10 ikiwa ni pamoja na "Paradise," ambayo ilichaguliwa kuwania tuzo za Booker na Whitebread mnamo 1994. Uzoefu wa ukimbizi na vurugu zinazoambatana nao ndiyo wazo kuu la sehemu kubwa ya kazi zake.

Chuo hicho kilinukuu kujitolea kwake kwa ukweli na kuchukia kwake urahisishaji wa mambo, kikisema riwaya zake "zinarejea nyuma kwenye maelezo na kufungua macho yetu kwa eneo utamaduni anuwai la Afrika Mashariki, ambalo ni geni kwa wengi katika maeneo mengine ya ulimwengu."

Afrika haijulikani kwa wengi katika sehemu zingine za ulimwengu. "

Tuzo ya Nobel ya Fasihi ndiyo nishani ya kifahari zaidi ya fasihi ulimwenguni, na inaambatana na zawadi ya pesa takribani dola milioni 1.1. Wateule wa chuo hicho wamekosolewa huko nyuma kwa kuwa watu wenye mitizamo tu ya kimagharibi, wakikosa anuwai na kwa kuwa na ajenda ya kisiasa.

Gurnah ndiye mshindi wa sita wa Afrika wa tuzo hiyo, akiungana na wengine kama Albert Camus, Wole Soyinka na J.M Coetzee.

Mwaka uliyopita, mshairi wa Kimarekani Louise Gluck alitunukiwa nishani hiyo, na kuwa moja wa wanawake 16 walioipata tangu mwaka 1901.

Chanzo: DPAE

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW