1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtanzania wa kwanza kuiongoza WHO-Afrika

28 Agosti 2024

Mbunge wa Kigamboni, na aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya Tanzania, Dokta Faustine Ndugulile amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani, Kanda ya Afrika.

Dr. Faustine Ndugulile
Mbunge wa Kigamboni, na aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya Tanzania, Dokta Faustine Ndugulile Picha: Ministry of health Tanzania

Dk Ndugulile, ambaye amechaguliwa katika mkutano mkuu wa kamati ya Shirika la Afya Duniani, WHO anakwenda kuiwakilisha Afrika katika sekta ya afya katika wakati ambapo Afrika inakabiliana na mzigo wa mlipuko wa homa ya Mpoxambayo imetajwa kuwa dharura ya afya ya umma kimataifa.

Dk Ndugulile ambaye anakuwa Mtanzania wa kwanza kuishika nafasi hiyo ya juu ya uongozi WHO, anakwenda kuliwakilisha bara la Afrika ambalo bado linakabiliwa na uhaba wa vifaa tiba, vifo vya uzazi na changamoto kubwa ya watanzania katika matumizi ya bima ya afya.Africa CDC yaitangaza mpox kuwa dharura ya afya ya umma

Mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Dk Ndugulile alituma ujumbe mfupi na kusema kwamba; "Ni heshima kwangu na kwa unyenyekevu ninafurahi kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi wa WHO kwa Afrika. Nawashukuru nchi wanachama kwa uaminifu mlioonyesha kwangu. Ninaahidi kufanya kazi nanyi na naamini kwamba kwa pamoja tunaweza kujenga Afrika yenye afya. Kwa Mkurugenzi Mkuu wa WHO, asante kwa kazi kubwa na ya mfano unayofanya, ninatarajia kushirikiana na wewe ili kuipeleka mbele ajenda ya afya, katika bara la Afrika".

Dr. Faustine Ndugulile(kulia) na mkurugenzi wa WHO duniani Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus(kushoto)Picha: Ministry of health Tanzania

Miongoni mwa ilani zake kuu zinazojikita katika nafasi yake ni kuwa na Ofisi Sikivu ya WHO Afrika, kuainisha afya na siasa, kuwezesha haki ya afya na kuwezesha utayari wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko Afrika.

Hata hivyo, wapembuzi yakinifu wa masuala ya afya wanasema, kuchaguliwa kwa Dk Ndugulile ni hatua nzuri kwa nchi kwani anakwenda kuwa balozi katika nchi zote za Afrika na kuliwakilisha bara la Afrika. Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani ya mwili, Elisha Osati, ameiambia DW. “Mimi sioni kama ni mzigo, lakini nadhani ni hatua nzuri kwake lakini pia kwa nchi, anakuwa kama balozi wetu Kwenye nchi zote za Afrika, lakini pia anatuwakilisha kwenye bodi ya juu sana ya WHO, lakini pia na umoja wa mataifa, kwa maana yek anaongeza visibility kwetu, akifanya vizuri zaidi anaweza kuongeza uwekezaji kwenye eneo la afya”

Mdau wa afya kutoka Wizara ya Afya, ambaye kwa nyakati tofauti amewahi kufaya kazi na Dk Ndugulile,  DK Katanta Msole, alikuwa na haya ya kusema baada ya ushindi huo. Taasisi ya CDC- Afrika yasema mataifa yasiokuwa na aina ya virusi vya Afrika Kusini yatumie chanjo ya AstraZeneca

Katika mkutano  huo uliofanyika nchini Congo Brazaville, Dk Ndugulile alikuwa akichuana na Dk Boureima Hama  Sambo wa Niger, Dr Ibrahima Soce Fall wa Senegal na Dk Richard Mihigo wa Rwanda. Bado Mkurugenzi huyu wa WHO Afrika atakwenda kuthibitishwa kamili, kushika nafasi hiyo katika sesheni ya 156 ya wakurugenzi wa bodi ya WHO, Februari, 2025. Geneva, Uswisi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW