Mtawala wa Nzuwani apuuza vikwazo vya Umoja wa Afrika
12 Oktoba 2007Matangazo
Moroni
Rais wa kisiwa cha Nzuwani,anaeshindana na serikali kuu ya visiwa vya Komoro tangu miezi sita iliyopita,Mohammed Bakar ,amesema vikwazo vinavyopangwa kuwekwa dhidi yake havitasaidia.Kutokana na maombi ya rais wa shirikisho la visiwa vya Komoro Ahmed Abdallah Mohammed Sambi,Umoja wa Afrika umesema jumatano iliyopita unatathmini uwezekano wa kupitisha vikwazo dhidi ya Nzuwani ili kumlazimisha Mohammed Bacar ang’oke madarakani,baada ya uchaguzi unaobishwa wa June iliyopita.”Uamuzi wa Umoja wa Afrika hautasaidia kitu,utatulazimisha tuzidishe makali ya msimo wetu” amesema hayo kanali Mohammed Bakar katika mahojiano ya simu na shirika la habari la Reuters.