Mtazamo wa vyama vya upinzani nchini Tanzania kuhusu swala la Zimbabwe
1 Julai 2008Katika mkutano wa viongozi wa Afrika unaoendelea huko nchini Misri Umoja wa mataifa na viongozi wa Umoja wa Afrika wamemtaka rais Mugabe kukaa kwenye meza ya mazungumzo na mpinzani wake Morgan Tsvangirai kufikia makubaliano ya kisiasa.Wakati huohuo waziri mkuu wa Kenya ameutaka umoja huo wa Afrika kumuondoa mugabe katika jumuiya hiyo.Haya yote yamezungumzwa wakati waangalizi wa uchaguzi kutoka jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC wakitoa taarifa yao iliyosema kwamba uchaguzi haukuwakilisha imani ya wazimbabwe.waangalizi wa umoja wa Afrika nao wamesema uchaguzi haukufikia viwango vilivyowekwa na nchi 53 za jumuiya hiyo.
Chini ya mkutano huo wa viongozi wa Afrika unaoendelea nchini Misri Je wapinzani barani Afrika wanautazama vipi mzozo wa Zimbabwe?Nimezungumza na Dkt Sengendo Mvungi aliyewahi kuwa mgombea wa urais wa chama cha NCCR Mageuzi nchini Tz.Na kwanza alikuwa na haya ya kusema.