Mtihani kwa chama cha AfD uchaguzi jimbo la Thuringia
27 Oktoba 2019Hali hii inakuja kufuatia shambulio la kigaidi lililofanywa na mfuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia mwezi huu dhidi ya sinagogi tukio ambao lilizusha wimbi la mshituko nchi nzima.
Uungaji mkono wa chama cha AfD katika jimbo la Thuringia kwa sasa uko kati ya asilimia 20 na 24, kwa mujibu wa uchunguzi wa hivi karibuni wa maoni ya wapiga kura, hali ambayo inaweza kusababisha chama hicho kinachopinga wahamiaji kuibuka kuwa nguvu ya pili kubwa katika bunge la jimbo hilo.
Wakati uungaji mkono wa chama cha AfD umechupa kutoka asilimia 10.6 katika uchaguzi wa taifa mwaka 2014, uungwaji wake mkono kwa sasa unaonekana kuwa chini kwa kile chama hicho ilivyopata katika jimbo hilo mwezi Agosti na Septemba.
Viongozi wa kisiasa nchini Ujerumani wamejiunga na makundi ya Wayahudi katika kulalamikia shambulio hilo la chuki dhidi ya wayahudi hapo Oktoba 9 katika jimbo jirani la Saxony-Anhalt kwa kiasi fullani katika chama hicho cha AfD.
Kamishna wa serikali anayehusika katika mapambano kupinga chuki dhidi ya Wayahudi amekishutumu chama cha AfD wakati akiidhinisha kile kinachofahamika kama "misimamo mingi ya kupiga chuki dhidi ya Wayahudi" wakati wengine walikifananisha na Wanazi mamboleo. Chama cha AfD binafsi kimeshutumu shambulio hilo la risasi kuwa ni "uhalifu mkubwa".
Uchunguzi wa maoni unaonesha kuwa waziri mkuu maarufu wa Thuringia Bodo Ramelow anaweza kupata uungwaji mkono wa kutosha kurejea madarakani baada ya kuwa kiongozi wa kwanza mwaka 2014 kutoka chama cha siasa kali za mrengo wa kushoto cha Die Linke kuongoza serikali ya jimbo nchini Ujerumani.
Lakini kutokana na hali ya wasi wasi kabla ya uchaguzi kulikuwa na madai kutoka kwa viongozi wa kisiasa wa chama katika jimbo hilo, ikiwa ni pamoja na Mike Mohring, kiongozi wa chama cha kansela Angela Merkel cha CDU katika jimbo hilo kuwa wamepokea vitisho kutoka kwa watu wenye msimamo mikali ya mrengo wa kulia.