1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Mtoto wa Museveni asema hatowania urais 2026

21 Septemba 2024

Mtoto wa kiume wa Rais Yoweri Museveniwa Uganda, ambaye alisema atawania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka 2026, ametangaza leo Jumamosi kwamba hatogombea na badala yake atamuunga mkono baba yake.

Uganda Entebbe 2024 |Muhoozi Kainerugaba
Muhoozi Kainerugaba,Mkuu wa Majeshi wa UgandaPicha: Ugandan Presidential Press Unit

Mtoto wa kiume wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda, ambaye alisema atawania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka 2026, ametangaza leo Jumamosi kwamba hatogombea na badala yake atamuunga mkono baba yake. 

Muhoozi Kainerugaba ambaye wengi wanaamini anaandaliwa kumrithi baba yake, ametangaza kupitia ukurasa wa mtandao wa X kwamba hatokuwemo kwenye sanduku la kura uchaguzi ujao.

Soma zaidi. Waganda watoa heshima za mwisho kwa mwanariadha Cheptegei

Mtoto huyo wa rais Museveni ambaye sasa anashikilia wadhifa wa Mkuu wa Majeshi wa Uganda amesema atamuunga mkono baba yake anayeitawala nchi hiyo ya Afrika Mashariki tangu mwaka 1986.

Museveni mwenyewe bado hajatangaza iwapo atawania muhuka wa 7 madarakani ifikapo 2026. Kainerugaba alisema hapo kabla dhamira yake ya kuwania urais ni kuwezesha damu changa kuongoza siasa za nchi hiyo.