1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu mmoja amekufa kwenye maandamano Venezuela

Josephat Charo
30 Julai 2024

Mtu mmoja amekufa kwenye maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jumaili iliyopita nchini Venezuela yaliyompa ushindi rais Nicolas Maduro wa asilimia 51.2 ya kura.

Caracas ya Venezuela | Maandamano ya kupinga kuchaguliwa tena kwa Rais Nicolas Maduro
Waandamanaji wakichoma mpira wakati wa maandamano ya kupinga kuchaguliwa tena kwa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro kwa muhula wa 3 baada ya uchaguzi wa urais wa Venezuela huko Caracas, Julai 29, 2024.Picha: Pedro Rances Mattey/Anadolu/picture alliance

Kifo hicho kiliripotiwa katika jimbo la kaskazini la Yaracuy, ingawa maelezo ya kina hayakufahamika, huku vyombo vya habari vya eneo hilo vikiripoti vifo vya watu angalau wawili. Shirika lisililo la kiserikali la Foro Penal limeandika kwenye mtandano wa kijamii wa X jana Jumatatu kwamba maandamano zaidi yamepangwa kufanyika hivi leo. Upinzaniumesema una ushahidi ulishinda uchaguzi na umeitisha maandamano makubwa leo dhidi ya serikali. Upande wa serikali nao unapanga kuwaleta wafuasi wake mabarabarani kukabiliana na wapinzani. Shirika la Foro Penal limesema watu wapatao 46 walikamatwa katika miji mbalimbali na majimbo ya nchi hiyo ya Amerika Kusini.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW