1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu mmoja ameuwawa katika maandamano Kenya

8 Julai 2023

Mtu mmoja ameuwawa kwa kupigwa risasi nchini Kenya katika maandamano ya kupinga ongezeko la gharama ya maisha na nyongeza yenye utata ya kodi.

Kenia Proteste der Opposition in Nairobi
Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Kulingana na Alex Ochieng, msimamizi katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Jaramogi Oginga Oginga mjini Kisumu, Mtu mmoja amefariki kutokana na majeraha ya risasi.

Soma pia: Polisi Kenya yatumia nguvu kuziwua maandamano dhidi ya kodi

Hapo jana polisi ya Kenya iliufyatulia mabomu ya kutoa machozi msafara wa magari wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga baada ya kuhutubia umati wa watu katika Mji Mkuu Nairobi.

Odinga ametangaza mpango wa kukusanya saini milioni 10 kwa ajili ya kumuondoa madarakani Rais William Ruto aliyekuwa mpinzani wake mkuu katika uchaguzi uliopita.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamelaani hatua ya waandamanaji kukamatwa kiholela.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW