1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu mmoja auwawa Israel kufuatia shambulizi la droni

Sylvia Mwehozi
19 Julai 2024

Mtu mmoja ameuwawa mjini Tel Aviv, nchini Israel baada ya jengo lililo karibu na ubalozi wa Marekani kushambuliwa na ndege isiyo na rubani.

Athari za shambulio la droni mjini Tel Aviv, Israel
Athari za shambulio la droni mjini Tel Aviv, Israel.Picha: Ricardo Moraes/REUTERS

Taarifa ya shambulio hilo imethibitishwa na afisa wa jeshi la Israel aliyekiri kuwa makosa ya kibinadamu, ndiyo sababu ya kushindwa kuizuia droni hiyo.

Kulingana na afisa huyo wa jeshi la Israel aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, droni yenye uwezo wa kusafiri masafa marefu ilishambulia majira ya saa tisa alfajiri.

Ameongeza kuwa, madhumuni makubwa ya shambulio hilo yalikuwa ni kuwauwa raia ndani ya Israel. Waasi wa Kihouthi wa Yemen wamethibitisha kuhusika na shambulio hilo.

Hayo yakijiri, bunge la Israel lilipiga kura jana kupinga taifa la Palestina linalochukuliwa kuwa kitisho, siku moja baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuwaambia wabunge kuwa jeshi limewakalia kooni wanamgambo wa Hamas.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW