1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Mtu mmoja auwawa katika shambulizi la Urusi nchini Ukraine

Josephat Charo
26 Septemba 2024

Urusi imefanya mashambulizi ya kutokea angani usiku wa kuamkia leo nchini Ukraine na kumuua mtu mmoja na kuharibu miundombinu muhimu.

ARCHIV | Ukraine Wuhledar | Beschädigte Gebäude in der Region Donezk
Majengo yaliyoharibiwa kufuatia mashambulizi ya Urusi katika mji wa Vuhledar Picha: Ozge Elif Kizil/Anadolu/picture alliance

Jeshi la anga la Ukraine limesema vikosi vya Urusi vilifanya mashambulizi 78 ya droni na makombora sita katika maeneo mbalimbali kote nchini wakati wa shambulizi lililodumu kwa muda wa masaa kadhaa.

Jeshi pia limesema mifumo ya ulinzi wa makombora umeziharibu droni 66 na makombora manne.

Soma pia: Zelensky asema hakuna mazugumzo ya amani ya Urusi 

Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine Ihor Klymenko, ameandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba mwanamke mmoja ameuwawa katika shambulizi la kombora huko Odesa kusini mwa Ukraine na watu wengine wanane wamejeruhiwa katika shambulizi la bomu kwenye mji wa Zaporizhzhia, kusini mashariki mwa nchi.

Droni kadhaa zimeharibiwa katika anga la mji mkuu Kiev ambako magari 20 na bomba la gesi limeharibiwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW