1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu mmoja auwawa kwenye maandamano Bangladesh

Josephat Charo
27 Novemba 2024

Serikali ya mpito imesema imejitolea kwa dhati kuhakikisha kuna utangamano wa jamii nchini Bangladesh kwa gharama yoyote ile.

Kiongozi wa Wahindu Chinmoy Krishna akamatwa mjini Dhaka
Kiongozi wa Wahindu Chinmoy Krishna akamatwa mjini DhakaPicha: Rashed Hossain rabbi

Polisi nchini Bangladesh wamesema mtu mmoja ameuliwa nchini humo kwenye makabiliano kati ya vikosi vya usalama na wahindu waliokuwa wakiandamana kupinga kukamatwa kwa kiongozi wa kidini.

Chinmoy Krishna Das, kiongozi wa Wahindu mwenye mafungamano na chama cha kimataifa cha Krishna alitiwa nguvuni kutoka uwanja wa ndege mjini Dhaka siku ya Jumatatu kwa mashitaka kadhaa, ukiwemo uchochezi.

Kukamatwa kwake kulizua maandamano ya wafuasi wake katika mji mkuu Dhaka na mji wa Chittagong. Polisi wamesema wakili muislamu aliuliwa wakati wa maandamano nje ya mahakama ya mjini Chittagong.

Serikali ya mpito ya Bangladesh imeamuru uchunguzi ufanyike kuchunguza mauaji hayo na vyombo vya usalama vimeelekezwa viimarishe usalama katika mji huo wa bandari.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW