Mtu mmoja auwawa na mabaki ya droni Urusi
9 Aprili 2026
Matangazo
Mabaki ya ndege isiyo na rubani iliyodunguliwa kusini mwa Krasnodar Krai yamemuua mwanamume mmoja. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gavana wa eneo hilo la UrusiVeniamin Kondratyev mapema leo.
Mwanamume huyo aligongwa na mabaki ya ndege isiyo na rubani alipokuwa kwenye roshani ya jengo la ghorofa katika kijiji cha Sauk-Dere katika wilaya ya Krymsk.
Vipande vya ndege zisizo na rubani zilizoharibiwa pia vilianguka kwenye eneo la biashara na katika maeneo kadhaa katika eneo hilo lakini hakuna majeraha yoyote yaliyoripotiwa.