1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Mtu na mkewe raia wa Marekani washtakiwa Uganda

22 Desemba 2022

Mahakama moja nchini Uganda imewashtaki mtu na mkewe raia wa Marekani kwa usafirishaji haramu wa watoto katika kesi ambayo huenda ikawatumbukiza watu hao katika kifungo cha maisha jela endapo watatiwa hatiani.

Lagos | Menschenhandel
Picha: PIUS UTOMI EKPEI/AFP

Mackenzie Leing Mathias Spencer na Nicholas Spencer walifikishwa katika mahakama ya Buganda Jumatatu wakidaiwa kumtesa na kumshikilia mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 10 katika chumba kidogo kilichokuwa na baridi akiwa mtupu bila nguo.

Nyaraka zilizofikishwa mahakamani zimeonesha watuhumiwa hao walimchukua mtoto huyo, kumsafirisha na kumshikilia mtoto huyo wa kumlea kwa lengo la kumtumikisha.

Awali mtu na mkewe walishtakiwa kwa kusababisha mateso na kudaiwa kumfungia katika chumba kidogo kilichowekwa kamera za kufuatilia kile kilichoelezwa kuwa mienendo na tabia zake za utundu. Watu hao bado wanashikiliwa rumande.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW