1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiKenya

Mtuhumiwa kinara wa ujangili Kenya apandishwa kizimbani

17 Septemba 2025

Waendesha mashtaka nchini Kenya jana wamempandisha kizimbani mwanaume mmoja aliyekamatwa kwa tuhuma za kuuza pembe mbili za Faru zenye thamani ya dola za kimarekani 63,000.

Faru| Ujangili | Uhifadhi| Kenya
Faru na Ndovu ni wanyama wanaolengwa na majangili ili kupata pembe zao. Picha: AP

Mwanaume huyo Feisal Mohammed Ali anakabiliwa na mashtaka hayo mapya ikiwa ni miaka tisa tangu alipotiwa hatiani kwa kuhusika na biashara ya pembe na vipusa kabla ya baadae kuachiwa huru.

Yeye na mshtakiwa mwenzake Mohammed Hassan walikamatwa kwenye mji wa mwambao wa Mombasa mwezi uliopita. Walipofikishwa mahakamani jana, wote wawali wameyakana mashtaka ya kuuza nyara za wanyama walio hatarini kutoweka.

Feisal alihukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani mwaka 2016 kwa kusafirisha pembe za ndovu lakini aliachiwa huru kupitia kesi ya rufaa mwaka 2018. Polisi inamtuhumu kuwa nyuma ya mtandao mpana wa ujangili uliosababisha mauaji ya karibu tembo 120.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW