1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Mtuhumiwa wa mashambulizi ya Bondi ashitakiwa kwa mauaji

17 Desemba 2025

Mwanaume anayetuhumiwa kufanya mashambulizi katika ufukwe wa Bondi mjini Sydney, Australia ameshtakiwa kwa makosa 59 yakiwemo mashtaka 15 ya mauaji.

Australien Sydney 2025 | Mauaji ya Ufukwe wa Bondi
Mtuhumiwa wa mashambulizi ya Bondi Australia ashitakiwa kwa mauajiPicha: The Bondi Reporter/Bestimage/IMAGO

Naveed Akram, mwenye umri wa miaka 24 ameshtakiwa baada ya kuamka kutoka kwenye hali ya kutokuwa na fahamu katika hospitali moja ya Sydney, Australia alikopelekwa baada ya polisi kumpiga risasi pamoja na baba yake ili kuwadhibiti wasiendelee kufanya mauaji.

Baba yake Sajid Akram, mwenye umri wa miaka 50 alifariki katika eneo la tukio.

Haya yanajiri wakati ambapo mamia ya waombolezaji wakianza shughuli za maziko ya wapendwa wao walioangamia wakati watu wenye silaha walipofyatua risasi katika sikukuu ya Wayahudi ya Hannukah katika ufukwe huo.

Watu 15 waliuwawa huku wengine zaidi ya 30 wakijeruhiwa vibaya na bado wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini. Inadaiwa kuwa watu wote waliouwawa walikuwa Wayahudi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW