1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda afutiwa mashitaka

13 Oktoba 2024

Mfanyakazi wa zamani wa Umoja wa Mataifa na kiongozi wa waasi wa Kihutu Callixte Mbarushimana amefutiwa mashitaka nchini Ufaransa.

Picha na mafuvu ya wahanga wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda
Picha na mafuvu ya wahanga wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini RwandaPicha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Mahakama moja mjini Paris imetangaza kuhitimishwa kwa kesi hiyo kwa kukosa ushahidi wa kutosha kwenye kesi hiyo, ikisisitiza kuwa hakuna taarifa zozote ambazo ziliwezesha kuthibitisha kwa uwazi kuwa mtuhumiwa alijihusisha na vitendo vya uhalifu.

Callixte Mbarushimana, mwenye umri wa 61 na aliyeshtakiwa tangu mwaka 2010 kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu amekuwa akikanusha mashitaka hayo na kusema hana hatia yoyote. Baada ya  mauaji ya kimbari , Callixte Mbarushimana aliikimbia Rwanda na kisha kupewa hadhi ya ukimbizi nchini Ufaransa mwaka 2003.