Mtuhumiwa wa shambulio la Berlin ni raia wa Pakistan
20 Desemba 2016Kijana wa miaka 23 amekamatwa akituhumiwa kuhusika na shambulio dhidi ya soko la X-Mas mjini Berlin. Polisi wanasema tukio hilo limefanywa makusudi. Wanasema walikuwa wakimjua mtuhumiwa kwa makosa madogo madogo. Anatajwa kuwa mkimbizi wa kutoka Pakistan aliyekuwa akiishi katika kambi ya wakimbizi ya Tempelhof mjini Berlin. Gazeti la Bild linamtaja kijana huyo kuwa ni Naved B. Anasemekana ameingia Ujerumani kama mwaka mmoja uliopita.
"Wachunguzi wanaamini lori limelengwa makusudi dhidi ya umati wa watu waliokuwa wakitembea katika soko la X-Mas" amesema afisa mmoja wa polisi mjini Berlin. Ameongeza kusema wanachunguza uwezekano kama shambulio hilo ni la kigaidi.
wiri wa mambo ya ndani Thomas de Maizière alisema "kuna mengi yanayoonyesha kuwa ni "shambulio la kigaidi. "Sababau hasa hatuzijui kwa uhakika. Hatutopumua si mpaka kila kitu kinafafanuliwa. Nisingetaka kuzungumzia neno shambulio kwa sasa ingawa kila kitu kinaashiria hivyo." Amesema waziri wa mambo ya ndani Thom,as de Maizière.
Wizara ya mambo ya ndani ya serikali kuu ya Ujerumani imeamuru bendera zishushwe nusu mlingoti katika majengo yote ya serikali,na taasisi zote nyengine kote nchini.
Mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa mambo ya ndani wa serikali za majimbo Klaus Bouillon anazungumzia kuhusu "hali ya vita kufuatia shambulio la Berlin.
Kansela Angela Merkel anapanga kuhutubia taifa wakati wowote kutoka sasa.
Wakati huo huo viongozi wa makanisa na wawakilishi wa dini zote nchini Ujerumani wanapanga kusimamia ibada maalum kuwakumbuka wahanga wa shambulio la Berlin.
Mwandishi:Hamidou Oumilkheir/dpa/Reuters/AFP/KNA
Mhariri: Iddi Ssessanga