1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshukiwa wa shambulizi la bunduki Marekani akutwa amekufa

28 Oktoba 2023

Mshukiwa wa shambulizi la bunduki lililowauwa watu 18 na katika jimbo la Maine nchini Marekani amepatikana akiwa amekufa kwa kile maafisa wa usalama wamesema kuwa alijipiga mwenye risasi.

Polisi wakiwa katika njia ya kuelekea nyumbani kwa mtuhumiwa wa mauaji ya Oktoba 26
Polisi wakiwa katika njia ya kuelekea nyumbani kwa mtuhumiwa wa mauaji ya Oktoba 26Picha: Joe Raedle/Getty Images

Mshukiwa wa shambulizi la bunduki lililowauwa watu 18 na katika jimbo la Maine nchini Marekani amepatikana akiwa amekufa kwa kile maafisa wa usalama wamesema kuwa alijipiga mwenye risasi.

Mkuu wa usalama wa jimbo la Maine Mike Sauschuck amearifu kuwa mwili wa mwanaume huyo aliyetambulishwa kwa jina la Robert Card ulipatikana usiku wa kumkia leo baada ya msako mkali wa siku mbili uliohusisha mamia ya polisi na idara nyingine za usalama.

Soma zaidi: Biden ataka silaha za mashambulizi zipigwe marufuku

Inaaminika kuwa Card ndiye mhusika wa shambulizi baya kabisa la bunduki lililotokea jioni ya siku ya Jumatano kwenye kituo kimoja cha michezo na mkahawa vilivyopo kwenye mji wa Lewiston. Mbali ya vifo vya watu 18 wengine 13 walijeruhiwa.

Rais Joe Biden amesema shambulizi hilo limeleta maafa kwa taifa zima na kurejea dhamira yake ya kulitaka bunge la nchi hiyo kuondoa tofauti za vyama ili lipitishe sheria kali za kukomesha uhalifu wa kutumia silaha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW