1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muafaka wa Uturuki na Falme za Kiarabu watuliza mizozo

8 Septemba 2021

Muafaka kati ya mahasimu wa kikanda Uturuki na Umoja wa Falme za Kiarbu umetuliza mvutano uliochochea mizozo ikiwemo vita nchini Libya, baada ya miaka kadhaa ya uhasama na matusi, wanasema maafisa na wanadiplomasia.

Türkei Ankara | Treffen Präsident Erdogan und Sicherheitsberater der VAE Scheich Tahnoun bin Zayed Al Nahyan
Picha: Presidential Press Office/REUTERS

Lakini wakati ambapo tofauti za kisiasa zikikita mizizi, mataifa hayo mawili yanatarajiwa kujielekeza kwenye kujenga uhusiano wa kiuchumi na kupunguza, kuliko kutatua mpasuko wa kiitikadi ulioigawa kanda ya Mashariki ya Kati.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mtawala halisi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mrithi wa Ufalme Mohammed bin Zayed al-Nahyan, walizungumza kwa njia ya simu wiki iliyoita kufuatia mawasiliano kati ya mafisa wa intelijensia pamoja na serikali.

Erdogan ambaye mwaka uliopita alisema Uturuki ingevunja uhusiano wa kidiplomasia na Abu Dhabi, baada ya taifa hilo kuanzisha uhusiano na Israel, pia alijadili uwekezaji wa UAE nchini Uturuki pamoja na mshauri wa taifa wa usalama wa Abu Dhabi.

Hatua zinakwenda kuliko walivyofikiria wengi

Afisa mmoja wa Emarati alisema UAE inatafuta njia za kuimarisha uhusiano, na kuzungumzia fursa za uwekezaji katika sekta za usafirishaji, afya na nishati. Mazungumzo kati ya Erdogan na al-Nahyan yanafuatia juhudi za awali za Uturuki kuzuliza mvutano na washirika wa UAE, Saudi Arabia na Misri. Mawasiliano hayo yameleta tija kidogo mpaka sasa, lakini baadhi wanaona hatua za UAE kuwa za haraka.

Ramani ya nchi za Uturuki na Falme za Kiarabu

Mwanadiplomasia moja wa Ghuba alisema hatua hizi zinakwenda haraka kuliko watu wengi walivyofikiria, na kwamba mataifa hayo yamebadili ukurasa.

Afisa mwandamizi wa Uturuki aliyaelezea mazungumzo ya Erdogan na Sheikh Mohammed kama hatua muhimu kuelekea kutatua mizozo ambayo imeukumba uhusiano wao, na kusema mataifa hayo mawili huenda yakafanya kazi pamoja katika kanda ya Mashariki ya Kati.

Lakini kwanza kutakuwa na hatua zitakazochukuliwa katika muktadha wa kiuchumi, alisema aifa huyo. Masuala mengine hayajaafikiwa, lakini shauku ilijengwa kukabiliana na sehemu kubwa ya matatizo hayo.

Mpasuko kati ya mataifa hayo una mizizi yake katika vuguvugu la mapinduzi ya umma ya mataifa ya Kiarabu, wakati Uturuki ilipounga mkono kundi la Udugu wa Kiislamu na washirika wao wa Kiislamu dhidi ya tawala za kiimla kuanzia Tunisia hadi Syria -- hatua iliyowashtua watala wa himaya ya Umoja wa Falme za Kiarabu, wanaouona Udugu wa Kiislamu kama kitisho cha kisiasa na kiusalama.

Uturuki pia iliiunga mkono Qatar katika mzozo wa Ghuba, na kuweka katika msuguano na UAE, Saudi Arabia na Misri, huku uungaji mkono wa Uturuki mwaka uliyopita, uliisaidia serijali ya Libya inayotmbuliwa na Umoja wa Mataifa kuvirejesha nyuma vikosi vilivyoungwa mkono na UAE vilivyokuwa vinajaribu kuukamata mji mkuu wa Tripoli.

Ni kweli kwamba mzozo umegharimu chumi

Mataifa hayo pia yameshtumiana kwa uingiliaji mbali na mipaka yao, na Erdogan wakati mmoja alimkaripia waziri wa mambo wa nje wa UAE kwa kumuelezea kama mtu wa hadhi ya chini alietajirika, baada ya waziri huyo kunakili ujumbe wa Twtter uliokosoa vikosi vya himaya ya ottoman - ambayo ndiyo mtangulizi wa taifa la sasa la Uturuki.

Nchini Somalia, Uturuki na Umoja wa Falma za Kiarabu zimeshindania ushawishi. Nchini Syria, Uturuki bado inawaunga mkono wapiganaji wanaompinga rais Bashar al-Assad, wakati UAE, ambayo wakati mmoja iliunga mkono waasi, imefungua tena ubalozi wake mjini Damascus.

Mahasimu kusitisha mapigano Libya

01:53

This browser does not support the video element.

Mafisa wa Uturuki na wanadiplomasia wa kanda ya Ghuba wanasema mataifa yote yanatambua ukweli kwamba mzozo wao umegharimu chumi zao na gharama hizo zimechochewa na janga la Covid-19. Gharama hiyo ilihisiwa hasa na Erdogan nchini Uturuki, ambako mfumuko wa bei wa asilimia 19 umepandisha pakubwa gharama za maisha.

Ingawa hakuna makubaliano yaliotangazwa kuhusu uwekezaji, mataifa hayo mawili tayari yanalo jukwaa la kiuchumi la kujengea. Tofuati na Saudi Arabia, ambayo inaendeleza ususiaji usio rasmi wa bidhaa za Uturuki, UAE inasema Uturuki inaendelea kuwa mshirika mkuu wa biashara wa kikanda.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW