MUBARAK NA AL-ASSAD WAKUTANA:
25 Desemba 2003Matangazo
CAIRO: Rais Hosni Mubarak wa Misri na mwenzake wa Syria Bashar al-Assad,baada ya kuwa na mkutano mfupi nchini Misri,wametoa muito kuwa eneo la Mashariki ya Kati lisiwe na silaha zo zote za maangamizi.Bila ya kugusia mradi wa silaha za kemikali na biolojia,ambao Marekani inaituhumu Syria kuwa inao,viongozi hao wawili walizitaja silaha za kinyuklia za Israel ambazo nchi hiyo haikuzitangaza.Syria inakabiliwa na uwezekano wa kuwekewa vikwazo na Marekani kwa sababu ya kuyaunga mkono makundi yanayoipinga Israel na kwa kuendelea kuweka vikosi vyake nchini Libnani.Licha ya Syria kusema kuwa Israel ni kitisho kwake,nchi hiyo imeeleza kuwa ipo tayari kuanzisha tena majadiliano ya amani pamoja na Israel,yaliokwama zaidi ya miaka mitatu.
