1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya kuutafuta mkwamo wa kisiasa Niger yakwama

9 Agosti 2023

Juhudi za kidiplomasia za kuutatua mkwamo wa kisiasa nchini Niger ambako wanajeshi wamechukuwa madaraka kwa wiki ya pili sasa zinaonekana kukwama.

Niger, Niamey | General Abdourahmane Tchiani bei einer Kundgebung von Anhängern der Putschisten
Picha: Balima Boureima/AA/picture alliance

Watawala wapya wa kijeshi wamekataa kukutana na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS.

Serikali ya kijeshi ya Niger imeendelea kukaidi shinikizo la kimataifa siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa mataifa ya ECOWAS, ambao utazungumzia uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi.

Niger yaukataa ujumbe wa upatanishi wa Umoja wa Mataifa

Uamuzi huo umezima matumaini ya mwisho yaliyokuwepo ya kuupatia mzozo huo suluhisho la kidiplomasia, na kuzua wasiwasi wa kutanuka kwa mgogoro huo kutokea taifa lenye eneo kubwa kabisa ukanda wa Sahel na lenye uzoefu wa matukio ya mapinduzi na uasi wa makundi ya Kiislamu.

Mali na Burkina Faso, ambazo pia zinaongozwa na wanasheria, hapo jana zililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzuia hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya Niger, zikisema kwenye barua yao kwamba hatua kama hiyo itakuwa na matokeo mabaya na inaweza kuivunja jumuiya ya ECOWAS.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW