Mudavadi amteua mgombea mwenza
22 Januari 2013Matangazo
Hafla hiyo imefanyika katika makao makuu ya chama cha UDF mjini Nairobi siku moja baada ya vyama vya kisiasa kuwasilisha majina ya wagombea wao kwa tume ya uchaguzi nchini IEBC. Kura ya mchujo iliyokamilika mwishoni mwa wiki iliyopita ilikumbwa na vurugu huku ndugu wa Waziri Mkuu Raila Odinga wakijiondoa kwenye kinyang'anyiro cha Ugavana huko Kisumu na Siaya. Mwandishi wetu Alfred Kiti kutoka Nairobi na taarifa kamili. Kusikiliza taarifa hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Alfred Kiti
Mhariri: Josephat Charo