Muhammad Yunus aanza kuiongoza Bangladesh
9 Agosti 2024Matangazo
Yunus ameapa kuirejesha nchi hiyo ya kusini mwa Asia kwenye utawala wa kidemokrasia, baada ya maandamano ya wanafunzi kuupinduwa utawala wa miaka 15 wa Sheikh Hasina.
Mshindi huyo wa Nobel, ambaye alirejea nyumbani akitokea Ulaya muda mchache kabla ya kula kiapo cha kuiongoza Bangladesh, alisema anadhamiria kuilinda katiba na kuheshimuwa haki za kiraia.
Mchumi huyo mwenye umri wa miaka 84, alisema Bangladesh sasa imepata uhuru wake kwa mara ya pili.
Kwenye hotuba yake, aliwataka raia kutolipizana visasi na kuchukuwa hatua za kusonga mbele pamoja. Marekani, Umoja wa Ulaya na India zimeelezea utayarifu wao wa kufanya kazi pamoja na serikali ya mpito inayoongozwa na Yunus.