1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yunus atoa wito wa kuungana kuijenga upya Bangladesh

10 Agosti 2024

Kiongozi wa mpito nchini Bangladesh Muhammad Yunus ametoa wito wa kuvumiliana katika masuala ya imani za kidini wakati akimfariji mama aliyekuwa kimlilia mwanae baada ya kuuwawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano

Bangladesh | Muhammad Yunus  mjini Dhaka
Kiongozi wa mpito nchini Bangladesh Muhammad YunusPicha: Mohammad Ponir Hossain/REUTERS

Mama huyo alihuzunishwa na kisa cha mwanawe Abu Sayeed aliyeuwawa kwa kupigwa risasi katika maandamano makubwa yaliyohitimisha utawala wa miaka 15 wa Waziri Mkuu Sheikh Hasina. 

Yunus ambaye ni mshindi wa Tuzo ya amani ya Nobel, alirejea nchini kutoka barani Ulaya alikokuwa uhamishoni, ili  kuiongozi nchi yake kuelekea mageuzi ya kidemokrasia. Yunus amesema wajibu wake sasa ni kujenga Bangladesh mpya isiyokuwa na migawanyiko ya kidini.  

Yunus asifu ´ukombozi wa pili´ wa Bangladesh

Kazi kubwa itakayomkabili Yunus kwa sasa ni kurejesha umoja na amani pamoja na kuingoza nchi hiyo katika kuandaa uchaguzi mpya baada ya kuondolewa kwa Hasina. Hata hivyo mtoto wa kiume wa Hasina, Sajeeb Wazed amesema serikali iliyoko sasa sio halali. 

Serikali ya Sheikh Hasina aliye na miaka 76 inashutumiwa kwa matukio makubwa ya ukiukwaji wa haki za binaadamu ikiwemo mauaji ya kiholela ya maelfu ya wapinzani wake kisiasa. Hasina anasemekana kuitoroka nchi na kuimbilia nchini India.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW