Muhubiri ahukumiwa kifungo cha maisha jela Uingereza
30 Julai 2024Matangazo
Hukumu hiyo imetolewa siku chache baada ya muhubiri huyo kutiwa hatiani katika mahakama ya Woolwich Crown kwa kuwa mwanachama wa kundi lililopigwa marufuku lenye misimamo mikali la al-Muhajiroun, au ALM na kwa kuhamasisha uungwaji mkono wa kundi hilo. Jaji Mark Wall amesema Choudary mwenye umri wa miaka 57, anaongoza kikamilifu kundi la kigaidi linalowatia moyo vijana kujiingiza katika vitendo vya misimamo mikali. Kundi la ALM lilipigwa marufuku na serikali ya Uingereza mnamo 2010 kama kundi linalojihusisha na kufanya, kupanga au kuendeleza ugaidi.