Munich. Pope azuru jimbo akilozaliwa.
11 Septemba 2006Matangazo
Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki Pope Benedict wa 16 ameendesha misa ya wazi katika jimbo la kusini mwa Ujerumani mahali alikozaliwa la Bavaria.
Zaidi ya watu 250,000 wamehudhuria misa hiyo mjini Munich.
Pope Benedict ameonya jamii za kisasa kutoacha imani katika sayansi na tekonolojia kuwafanya viziwi kwa ujumbe wa Mungu, na kushauri kuwa mabara ya Asia na Afrika yanaweza kutoa mafunzo kwa mataifa tajiri juu ya imani.
Misa hiyo ni kati ya misa tatu zitakazofanyika katika maeneo ya wazi na Pope wakati wa ziara yake ya siku sita.
Hii ni ziara ya pili ya Benedikt kuizuru Ujerumani tangu kushika wadhifa huo mwaka jana.