Muqtada al Sadr atishia kutangaza vita dhidi ya serikali ya Iraq
20 Aprili 2008BAGHDAD
Kiongozi wa kidini wa madhehebu ya kishia Moqtada al Sadr ametishia kutangaza vita dhidi ya serikali ya Iraq ikiwa haitokomesha opresheni zake dhidi ya wafuasi wake.Sadr hapo jana ametoa ilani ya mwisho kwa serikali ya Iraq na kuitolea mwito kufuata njia ya amani.Matamshi ya kiongozi huyo wa kidini yametolewa wakati wanajeshi wa Iraq wakisaidiwa na vikosi vya Marekani na Uingereza walipopambana na jeshi la Mehdi mjini Baghdad na kusini mwa miji ya Nasiriya na Basra.Taarifa za vyombo vya habari zimeleeza kuwa mapigano ya Basra yalikuwa makali kabisa kuwahi kutokea tangu mwishoni mwa mwezi uliopita wakati serikali ilipoanzisha opresheni iliyoshindwa kufanikiwa ya kuwanyang'anya sialaha wafuasi wa Sadr na wanamgambo katika mji wa kusini wa bandari.