1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museven akataa mwanae kujiuzulu

Lubega Emmanuel9 Machi 2022

Utawala wa jeshi nchini Uganda umefahamisha kuwa Rais Yoweri Museveni amemkataza mwanae Jenerali Muhoozi Kainerugaba kujiuzulu.Hata hivyo jeshi limesema bado halijapokea taarifa rasmi kutoka kwa Jenerali huyo.

Uganda | Yoweri Museveni während Interview
Picha: ABUBAKER LUBOWA/REUTERS

 Msingi wa sakata hili unakuwa ni kiini cha kuendeleza mjadla  wa urithi wa kiti cha urais Uganda pamojana mitazamo kuwa familia ya Museveni huwabadili watu mawazo waache kufikiria kuhusu matatizo yao ya kila siku kama vile mfumko wa bei ya mafuta na chakula.

Tangu aliposambaza taarifa hapo jana kwamba anastaafu kwenye jeshi la nchi hiyo alipohudumu kwa miaka mingi, kamanda wa jeshi la nchi kavu jenerali Muhoozi Kainerugaba ameibua mijadala ndani na nje ya utawala wa babake.

Kile ambacho wengi wamehoji ni kwa nini hajafuata utaratibu wa utawala wa jeshi kuhusu suala hilo ambalo limekuwa nyeti kwa baadhi ya maafisa wa ngazi za juu ndani ya jeshi wanaohitaji kustaafu kwa hiyari kama vile David sejusa.

Sioma Pia:Mtoto wa Museveni azusha mjadala kwa kuiunga mkono Urusi

Jeshi nchini humo limetolea ufafanuzi suala hilo kwa hoja kuwa  hayo yalikuwa ni kama maoni yake na kuongeza kuwa bado halijapokea maombi rasmi kutoka kwake na wala hawezi kujiuzulu kwani amiri jeshi mkuu Jenerali Yoweri Museveni pia amemkataza kufanya hivyo.

Wachambuzi wakosoa hatua hiyo

Mchambuzi wa masualaya kisiasa John Kibego amesema hatua hiyo ni kama vile kukiuka nidhamu ya kijeshi kwani Jenerali huyo anaeshikilia wadhifa wa juu jeshini hakufuata utaratibu ambao jeshi umejiwekea katika suala zima la hiyari ya kuustaafu.

Raia wa Uganda wakiwa kwenye foleniPicha: Jerome Delay/AP/picture alliance

 Ameongeza inatafakarisha jeshi linae msemaji na limethibitisha kutopata taarifa zozote rasmi kutoka kwa jenerali Muhoozi, "hii inaleta wasiwasi mkubwa kuhusu msimamo wa serikali ya Uganda inavyooendesha mambo yake" Alisisitiza Kibego alipozungumza na DW

Soma Pia:Mjadala waibuka kuhusu mageuzi ya katiba nchini Uganda

Kwa upande wake  kiranja wa upinzani bungeni John Baptist Nambeshe emetaja kile alichokiita kuwa ni uvumi katika mitandao ya kijamii juu ya Jenerali huyo kuchukua nafasi ya baba yake Rais Museven kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi 2026 kimedhihirika sasa na tangazo lake la kuustafu ni kama sehemu ya kumuandaa kuwania wadhifa huo wa juu kabisa katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

"Anataka kuwa raia wa kawaida ili tume ya uchaguzi imuidhinishe kugombea Urais."

Muhoozi abadili wazo lake la kustaafu

Katika kanda nyingine ya video iliyosambazwa na marafiki zake saa kadhaa baada ya taarifa yake kujiuzulu kwenye jeshi, Jenerali Muhoozi anaonekena akisema kuwa amebadili nia yake na  atajiuzulu baada ya miaka minane.

Muhoozi Kainerugaba katika sherehe za kijeshiPicha: Joseph Kiggundu/Photoshot/picture alliance

Hii imeibua hoja kama utawala unazingatia kuwa masuala ya kisiasa yanapewa kipaumbele badala ya maisha magumu yanayowakabili wananchi kwa sasa kikiwemo mfumko wa bei ya mafuta na vyakula.

Mjadala kuhusu nani atakayemrithi rais Museveni huibukakila kukitokea wazo la mmoja kati ya watu wa familia yake wanaodhaniwa kuwa

wanandaliwa kushikilia wadhifa huo. Jenerali Muhozi ni miongoni mwa watoto wa rais Museven ambao wananyooshewa kidole kuwa miongoni mwa wanaoandaliwa kumrithi baba yake.