Museveni abadili msimamo wake kuhusu kufunguliwa shule
29 Oktoba 2021Awali Rais Museveni alisisitiza kuwa shule zisingefunguliwa hadi pale watu wote walio na umri wa miaka 18 kwenda juu watakapokuwa wamepata chanjo dhidi ya COVID-19. Lakini kadri serikali inavyofanya juhudi kuendesha zoezi hilo, kuna changamoto kadhaa ambazo zinatatiza watu wengi kuweza kupata chanjo. Sasa kiongozi huyo wa Uganda amebadili msimamo wake akisema kuwa lazima shule na sekta zingine za uchumi zifunguliwe mwakani, huku akiwaonya watu ambao hawajachanjwa watajilaumu wenyewe.
Kulingana na takwimu za shirika la Umoja Mataifa linalowashughulikia watoto, UNICEF, Uganda ndiyo nchi ya pekee barani Afrika ambako shule zingali zimefungwa kwa muda mrefu. Hadi sasa, shule zimefungwa kwa muda wa wiki 77 sawa na takriban miaka miwili ya masomo.
Soma piaUganda yakumbwa na mripuko wa pili katika siku mbili:
Shinikizo za ndani na kimataifa
Kumekuwepo shinikizo kutoka ndani na nje ya nchi kwa serikali ya Uganda kufungua shule, wazazi na wanajamii wakisema kuwa kuendelea kufungwa kwa shule kumesababisha madhara makubwa kwa watoto, hasa wale wa kike. Takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi hicho, zaidi ya wasichana laki moja wamepata mimba za utotoni na hata wengine sasa wanalea mimba ya pili. Watu mbalimbali wametoa maoni kuhusu hatua ya Rais Museveni kubadili msimamo wake:
Sababu nyingine ya idadi ndogo ya watu kupata chanjo hadi sasa ni uhaba wake. Serikali imekuwa ikisema iliagiza chanjo za kukidhi hadi watu milioni 23 lakini shehena hiyo bado haijawasilishwa.
Soma pia:Visa vya COVID 19 vyazidi kuenea Uganda
Kero za abiria kuhusu vipimo vya Covid-19
Kwingineko, abiria wanaondelea kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe wameshtumu hali ya kucheleweshwa wakisubiri matokeo ya kupimwa COVID-19. Zoezi hilo linalondeshwa na majeshi wakisaidiwa na madaktari lilianza mkesha wa siku ya Jumatano. Kanda ya video iliyosambazwa kwenye majukwaa ya kijamii ikionyesha abiria walioghabishwa na hali hii imesababisha shutuma nyingi na watu kuhoji kwa nini watu wapimwe hata wakiwa na hati halali. Mmoja kati ya abiria aliyezuiliwa anasimulia hivi.
Ijapokuwa Uganda imepokea dozi zaidi ya milioni tisa na nusu za chanjo dhidi ya COVID-19 ni chanjo milioni 2.9 tu ambazo zimetumiwa.