1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni: Afrika itafute suluhu ya matatizo yake yenyewe

Lubega Emmanuel. 12 Mei 2021

Rais Yoweri Museveni ambaye ameapishwa rasmi Jumatano kutawala nchi hiyo kwa miaka mingine mitano amekariri kuendelea kuhamasisha viongozi wa Afrika kutafuta suluhu ya matatizo ya bara hili badala ya kuwategemea wageni.

Uganda Kampala | Erneute Amtseinführung | Yoweri Museveni
Picha: Lubega Emmanuel/DW

Imekuwa ni shangwe na nderemo kwa wafuasi wa chama cha NRM wakati Jenerali Yoweri Museveni akiapa kutawala Uganda kwa awamu nyingine ya miaka mitano.

Hii ikiwa ni awamu yake ya sita tangu alipotwaa madaraka mwaka 1986, Museveni amekariri mwito wake kwa viongozi wa Afrika kuzingatia kutatua matatizo ya bara hili wao kwa wao badala ya kuwategemea wageni wanaotanguliza maslahi yao na kuwawekea masharti ya kuwapa misaada na mikopo.

Museveni ametoa mfano wa mataifa ya Afrika kuzidisha biashara kati yao akiwashukuru viongozi wa mataifa ambayo yamekubali bidhaa kutoka Uganda kuingia katika masoko yake.

Aliyekuwa mpinzani mkuu wa rais Museveni katika uchaguzi wa rais Bobi WinePicha: Emmanuel Lubega/DW

Akigeukia wananchi wa Uganda, Museveni ameahidi kuwa katika awamu hii ya miaka mitano atatilia mkazo suala la kuboresha mapato yao na ikiwezekana atakiuka taratibu za urasmi ambazo wakati mwingine kumkwaza kutekeleza mambo fulani.

Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kiuchumi wanaonya kuwa mikakati ya Museveni ya kuiweka nchi katika kiwango cha pato la kati kama alivyofanikiwa hayati Magufuli nchini Tanzania inahitaji mageuzi makubwa ya jinsi matumizi ya raslimali za serikali zinavyotumiwa.

Rais Museveni aapishwa kwa muhula wa sita.

01:33

This browser does not support the video element.

Paul Corti ni mtafiti wa masuala ya kiuchumi katika taasisi ya utafiti wa sera za kiuchumi katika Chuo Kikuu cha Makerere.Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla ya kuapishwa kwa Museveni ni pamoja na rais wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye licha ya kuwasili kuchelewa amehakikisha kuwa anashuhudia Museveni akitawazwa kuongoza Uganda hadi mwaka 2026.