Museveni aongoza katika matokeo ya awali Uganda
16 Januari 2026
Matangazo
Tume hiyo imesema Museveni anaongoza kwa takribani asilimia 76 ya kura zilizohesabiwa hadi sasa, ikilinganishwa na takribani asilimia 20 alizopata mpinzani wake mkuu, Bobi Wine.
Chama cha Bobi Wine, National Unity Platform, kimesema kuwa kiongozi wao amewekwa chini ya kizuizi cha nyumbani katika mji mkuu Kampala, madai ambayo polisi wamekanusha.
Bobi Wine, ambaye amekuwa sauti muhimu ya upinzani, amekuwa akilalamikia vitisho, kukamatwa kwa wafuasi wake na mazingira yasiyo huru ya kampeni. Mashirika ya haki za binadamu pia yameeleza wasiwasi kuhusu kiwango cha uhuru wa kisiasa wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi.
Endapo Museveni atathibitishwa mshindi, ataanza muhula wake wa saba madarakani tangu achukue uongozi mwaka
1986.