1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni apiga marufuku 'mitumba'

25 Agosti 2023

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amepiga marufuku uingizaji wa nguo za mitumba akisema unalemaza ustawi wa viwanda vya nguo vya nchi hiyo, akiziita nguo hizo kuwa "za watu waliofariki katika nchi za Magharibi."

Afrika, Mitumba | Gebrauchte Kleidungen
Picha: Felix Maringa/DW

Museveni aliyasema hayo siku ya Ijumaa (Agosti 25) katika hafla ya uzinduzi wa viwanda tisa katika eneo la viwanda la China na Uganda mjini Mbale.

Kama nchi nyingi za Afrika, Uganda imekuwa ikiagiza kiasi kikubwa cha nguo za mitumba ambazo baadhi ya wateja wanazipenda kwa kuwa bei yake ni nafuu.

Soma zaidi: Museveni akemea shinikizo la Benki ya Dunia kufuatia usitishwaji mikopo

Kulingana na shirika la Oxfam, karibu asilimia 70 ya mchango wa nguo kwa mashirika ya misaada Ulaya na Marekani inaishia Afrika.

Museveni amesema pia amepiga marufuku uagizwaji kutoka nje wa mita na nyaya za umeme akisema vifaa hivyo vinastahili kununuliwa katika viwanda vya Uganda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW