1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Museveni asaini sheria ya mapenzi ya jinsia moja

29 Mei 2023

Spika wa bunge la Uganda Anita Among, amewahimiza wale wanaohusika katika kahikikisha sheria hiyo inatekelezwa wanaweza kuendelea na shughuli hiyo.

Hata baada ya kurekebishwa, lakini vipengele vikali zaidi na vilivyopingwa na mataifa ya Magharibi bado vingalipo
Hata baada ya kurekebishwa, lakini vipengele vikali zaidi na vilivyopingwa na mataifa ya Magharibi bado vingalipoPicha: ABUBAKER LUBOWA/REUTERS

Mnano tarehe 2 mwezi huu, bunge la Uganda liliupitisha muswaada huo dhidi ya mapenzi ya jinsia moja na ushoga kwa jumla baada ya kuufanyia marekebisho kufuatia shinikizo la kimataifa. Awali muswaada huo ulikuwa umepitishwa tarehe 21 mwezi machi. Aprili 20 rais Museveni alishauri kwamba muswaada huo ufanyiwe marekebisho ili wale wanaostahili kuadhibiwa ni wahusika moja kwa moja katika vitendo hivyo na wale wanaowapotosha watoto kijiunga na mienendo hiyo.Hii leo imebainika kuwa muswaada huo sasa ni sheria baada ya kusainiwa na rais Museveni. Hata hivyo, mmoja kati ya watu wa jumuiya hiyo ya LGBTQ kanda ya Rwenzori Magharibi mwa Uganda amekosoa vikali hatua ya rais kurasimisha sheria hiyo. 

 '' Idhini ya rais kwamba muswaada huo sasa ni sheria nadhani itaathiri pakubwa maisha ya watu wa jumuiya ya LGBTQ sana na tunahofia sana kwamba hali inaenda kuwa mbaya sana'', alisema.

Sheria ya jinsia moja inamaana gani Uganda ?

Hatua hiyo inamaanisha kwamba kuanzia sasa watu wa jamii hiyo nchini Uganda watachukuliwa hatua zinazotajwa kuwa kali zaidi ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na hukumu ya kifoPicha: Anna Moneymaker/Getty Images

Katika taarifa aliyosambaza asubuhi ya leo kwa vyombo vya habari, spika wa bunge Anita Among amelezea sheria hiyo kuwa kielelezo chake yeye na wabunge wenzake kulinda hadhi, utamaduni na maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo. Amehimiza vyombo vya kisheria kuanza kutekeleza sheria hiyo ipasavyo. Mbunge Asuman Basalirwa ambaye aliwasilisha muswaada huo bungeni amefafanua hivi kuhusu kile kilichorekebishwa katika sheria husika akisisitiza kuwa adhabu kali zingali zinazingatiwa katika sheria hiyo.

 ''Ukimkuta mtoto au mtu aliye na ulemavu akiwa mwaathrika wa ushoga na usitoe taarifa, hiyo ni hatia.''

Lakini mwanaharakati na mmoja kati ya watu wa jumuiya hiyo ametoa kauli hii.

''Tunahisi hatujatenda  hatia yoyote kwa sababu mimi kuwa vile nipendavyo sidhani ni hatia. Tunaiomba serikali ya Uganda kuzingatia haki zetu sisi ni watu wazuri sisi ni waganda wazuri.''

Kinachosuburiwa sasa ni kuona jinsi mataifa ya Magharibi yatakavyoitikia hatua ya kusainiwa sheria hiyo. Kwa muda mrefu, serikali na wanaharakati watetezi wa jumuiya hiyo maarufu kama LGBTQ wamekuwa wakiishinikiza Uganda kutupilia mbali muswaada huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW