Museveni awaomba radhi viongozi wenzake
18 Mei 2011Matangazo
Siku hiyo, umati mkubwa ulikuweko uwanja wa ndege kumlaki kiongozi wa upinzani nchini humo, Kizza Besigye aliyekua akirejea nyumbani kutoka Nairobi alikokwenda kwa matibabu.
Kuwasili kwa Besigye katika siku ambayo Museveni alikuwa anaapishwa tena kuitawala Uganda, akiwa tayari ameshakaa madarakani kwa miaka 25, kulizusha machafuko katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu wa Kampala.
Museveni amesema gari la rais wa Nigeria lilipigwa mawe na lile la Rais wa Congo lilikaribia kufikwa na kisa kama hicho.
Amewataka radhi viongozi hao kutokana na kitendo hicho alichokiita kuwa cha kihuni na cha aibu kwa taifa la Uganda.
Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman
Mhariri: Mohammed Khelef