Museveni: Kupunguza ushuru kutavuruga mipango ya serikali
23 Mei 2022Akilihutubia taifa lake mwishoni mwa juma lililopita Museven alibainisha hayo na kuongeza kuwa, endapo serikali itachukua hatua hiyo ni wazi itachelewa kufikia lengo la kimaendeleo.
Hotuba ya rais Museveni kwa taifa kuhusiana na suala la mfumko wa bei za bidhaailisubiriwa kwa matarajio kuwa angetangaza mikakati ya kukabiliana na gharama za juu za maisha ambazo zimewakumba wananchi.
Hii ina maana kuwa raia wataendelea kuishi na hali iliyopo sasa ambapo kila kukicha bei za mafuta, chakula na ada mbalimbali zinapanda kwa kasi ya juu wakati mapato na mishahara ikibakia palepale.
Soma zaidi:Museveni akataa mwanae kujiuzulu
Museveni aliwataka wakaati wa taifa hilo la Afrika mashariki kuhakikisha wanabana matumizi katika mahitaji yao ya kila siku, huku akishikilia msimamo wa serikali yake kutopunguza kodi
"Tutumie vizuri pesa zetu na tujiepusha na uagizaji wa bidhaa kutoka nje" Alisema Museven kwenye sehemu ya hotuba yake.
Namna Hali ilivyo kwa sasa Uganda
Katika kipindi cha miezi mitatu sasa, bei za bidhaa muhimu za matumizi ya nyumbani zimepanda kati ya asilimia 50 na 300.
Bei za sabuni, mafuta ya kupika, unga na sukari ndizo zilizowaathiti zaidi raia wa kawaida ikiwemo wale wa vijijini. Nauli za usafiri na ada za usafirishaji bidhaa nazo zimepanda kwa kiwango kikubwa.
Baadhi ya wananchi waliiambia DW kuwa wamevunjwa moyo na hotuba ya rais Museven kwani walitaraji kupata faraja kutokana na namna bidhaa zilivyopanda.
"Nimevinjika moyo sana na hotuba ya rais,tilitarajia tupate majibu juu ya hali ilivyo" Mkaazi wa Kampala aliiambia DW.
Soma zaidi:Mkosoaji wa rais Museveni aitoroka Uganda
Walisema kuwa endapo serikali yao ingelipunguza bei ya mafuta ingelichochea kupungua kwa bidhaa zingine muhimu, ikiwemo vyakula,mafuta ya kupikia na hata usafiri.
Museven:Tunatumia kiasi kikubwa cha hazina ya fedha za kikegni kwa ajili ya mafuta
Rais Museveni alitoa angalizo kuwa kwa sasa Uganda inatumia kiasi kikubwa cha fedha zakeza kigeni kuagiza bidhaa hiyo na ikiuzwa kwa bei ya chini itakuwa na athari kwa uchumi wa nchi.
aliongeza kuwa mbali na kushusha kasi ya maendeleo ya taifa hilo kadhalika itachochea magendo ya bidhaa hiyo kwenye mipaka ya nchi kwa sababu bei ya mafuta itabaki ya juu katika mataifa jirani.
Soma zaidi:Wanaharakati Uganda wapinga washukiwa kuuawa
Wachambuzi wa masuala ya kijamii na kuichumi wana mtazamo kuwa Uganda imeiga mfano wa mataifa jirani Tanzania na Kenya ambako suala hilo limeshughulikiwa na sasa wananchi wanahisi nafuu kidogo.
Bidhaa zingine ambazo bei yake ilipanda na kukwaza mipango ya wananchi ya kujendeleza kimaisha ni zile za ujenzi. ikiwemo bei ya saruji kupanda kwa asilimia 40.