1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni: Ushindi unadhihirisha umaarufu wa chama changu

19 Januari 2026

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema jana kwamba ushindi wake wa kishindo katika uchaguzi wa rais uliokamilika siku chache zilizopita, unaonyesha umaarufu wa chama chake.

Uganda Kampala 2026 | akitoa hotuba wakati wa kampeini wa mwisho za chama chake mnamo Januari 13 mjini Kampala
Rais wa Uganda Yoweri MuseveniPicha: AFP

Siku moja baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo, Museveni amesema matokeo hayo yameonyesha uthabiti wa chama chake kinachojulikana kama National Resistance Movement.

"Upinzani ulikuwa na bahati, kwa sababu watu wangu milioni 10 hawakujitokeza. upinzani ungeaibishwa vibaya sana."

Katika hotuba yake hiyo, Museveni pia aliushtumu upinzani kwa kujaribu kuzua vurugu wakati wa upigaji kura.

Amewataka viongozi wa dini kuwashauri vijana ambao huenda wakapotoshwa kuzua vurugu.

Museveni amesema baadhi ya wapinzani wamekosea lakini pia ni magaidi huku akimtaja mpinzani wake wa karibu Bobi Wine na wengine kama wasaliti.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW