1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mustakabali wa FIFA baada ya Blatter kung'atuka

5 Juni 2015

Rais wa Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA, Joseph Sepp Blatter, ametangaza anajiuzulu Jumanne (02.06.2015) kufuatia kashfa ya rushwa kukikumba chombo hicho kinachosimamia mchezo wa kandanda.

Joseph Blatter
Picha: Reuters/A. Wiegmann

Blatter raia wa Uswisi mwenye umri wa miaka 79, na mlezi wake raia wa Bazil, Joao Havelange, wameiongoza FIFA tangu mwaka 1974, wakiyapa madaraka mashirikisho ya soka na wakuu wa kanda ambao waliwatii kikamilifu.

Lakini hayo yote huenda yakabadilika katika miezi michache ijayo, huku Blatter akiitisha uchaguzi mpya utakaoshawishi jinsi FIFA inavyoendeshwa, jinsi inavyofanya biashara na wadhamini, vyombo vinavyotangaza na kuonyesha kandanda, mashirikisho ya soka, ligi, vilabu, wachezaji na mawakala. Je FIFA inaelekea wapi? Na je upi mustakabali wa Blatter mwenyewe?

Jiunge na Josephat Charo katika kipindi cha Maoni mbele ya meza ya duara akiwa pamoja na Gwiji la michezo, Ramadhani Ali, katika mji wa Cologne, Ujerumani. Ramadhani Tuwa, mchambuzi wa michezo kutoka visiwani Zanzibar. Ramadhani Mtemi, mwanaspoti na pia mchambuzi wa masuala ya soka, jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Na Hussein Mohammed, meneja wa kampuni ya soka jijini Nairobi, Kenya inayoandaa michunao ya kandanda kwa vijana chipukizi mikoani.

Kusikiliza maoni bonyeza alama ya spika za masikio hapo chini.

Mwandishi:Josephat Charo

Mhariri:Iddi Sessanga

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi