1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Muungano tawala Japan wapoteza wingi wa viti bungeni

28 Oktoba 2024

Muungano tawala wa Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba umepoteza wingi wa viti katika bunge lenye viti 465 katika uchaguzi muhumu wa bunge uliofanyika Jumapili.

Japan Tokyo 2024 | Shinjiro Koizumi akizungumzia uchaguzi wa bunge
Chama cha LDP kimesema ni wakati wa kujitathmini na kutimiza matarajio ya wapiga kuraPicha: Takashi Aoyama/AFP

Chama cha Ishiba cha Liberal Democratic bado ndio chama kikuu katika bunge la Japan, na mabadiliko ya serikali hayatarajiwi. Lakini matokeo ya Jumapili yanaweka hali ya sintofahamu ya kisiasa. Kutokuwa na wingi wa viti kuna maana itakuwa vigumu kwa Waziri Mkuu Ishiba kupitisha bungeni sera za chama chake, na huenda akahitajika kumtafuta mshirika wa tatu katika muungano tawala.

Soma pia: Chama tawala Japan huenda kikaangushwa kwenye uchaguzi

Ishiba aliingia madarakani Oktoba mosi na maramoja akaitisha uchaguzi kwa matumaini ya kupata uungwaji mkono baada ya mtangulizi wake, Fumio Kishida, kushindwa kushughulikia ghahabu ya umma kuhusu kashfa za chama cha LDP.

Akizungumzia matokeo hayo, Waziri Mkuu Ishiba mwenye umri wa miaka 67, amesema anaamini wapiga kura wamekiambia chama kijitathmini na kuwa chama kinachotimiza matarajio yao.