1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Muungano wa Modi washinda wingi bungeni India

5 Juni 2024

Muungano wa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi umeshinda wingi bungeni katika uchaguzi wa nchini humo uliofanywa kwa awamu.

India Darbhanga | Waziri Mkuu Modi kwenye mkutano wa uchaguzi na Shambhavi Choudhary
Waziri Mkuu Narendra Modi akiwa na mgombea Shambhavi Chaudhary wakati wa mkutano wa Uchaguzi wa Lok Sabha Mei 4, 2024 huko Darbhanga, India.Picha: Santosh Kumar/Hindustan Times/IMAGO

Haya ni kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotangazwa mapema leo na tume ya uchaguzi nchini India. Hesabu rasmi imeonesha kwamba muungano huo wa National Democratic Alliance umeshinda viti 282 bungeni, hiyo ikiwa ni viti kumi zaidi ya vile vinavyohitajika ili kupata wingi katikabunge hilo. Idadi hiyo lakini ilikuwa ndogo ikilinganishwa na vile ilivyotabiriwa. Modi alikuwa tayari amedai kwamba ameshinda hapo jana ingawa matokeo rasmi yalikuwa hayajatolewa na chama chake cha BJP kilishinda viti 60 vichache kuliko ile rekodi ya viti 303 kilichoshinda katika uchaguzi wa mwaka 2019.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW