1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muungano wa upinzani Poland washinda nafasi ya Spika bungeni

Sylvia Mwehozi
14 Novemba 2023

Muungano wa vyama vinavyounga mkono Umoja wa Ulaya nchini Poland, umeshinda nafasi ya Spika wa bunge, baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Poland Warswa | Mkataba wa muungano wa upinzani wa sasa
Viongozi wa vyama vya upinzani vya kiliberali vya Poland (kuanzia wa pili kushto-kulia) Szymon Holownia na Wladyslaw Kosiniak Kamysz wa chama cha Third Way, Donald Tusk wa Civic Coalition, na Wlodzimierz Czarzasty na Robert Biedron wa chama cha Shoto wakitia saini mkataba wa muungano, katika bunge la Poland mjini Warsaw Novemba 10, 2023.Picha: WOJTEK RADWANSKI/AFP

Mgombea wa vyama hivyo Szymon Holownia amechaguliwa kwa kura 265 dhidi ya 193 za mgombea wa chama tawala cha Sheria na Haki PiS katika bunge lenye viti 460.

Ushindi huo unatizamwa na wengi kama jaribio la mwisho kwa vyama vitatu vya upinzani vinavyotafuta kuunda serikali mpya na kukiondoa chama cha kihafidhina cha Sheria na Haki PiS.

Soma pia: Muungano wa upinzani wafanikiwa wingi wa viti Poland

Kikao hicho cha kwanza cha bunge kimefanyika wakati pande zote mbili za upinzani na muungano wa chama tawala zikijaribu kuunda serikali.

Chama cha Sheria na Haki PiS kilishindwa kupata wingi wa viti bungeni kuweza kuunda serikali licha ya kushinda uchaguzi wa Oktoba. Lakini kilipewa nafasi ya kwanza ya kuunda serikali na Rais wa Poland Andrej Duda.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW