Vyama vya mrengo wa kushoto vyashinda uchaguzi Ufaransa
8 Julai 2024Muungano huo wa mrengo wa kushoto umejishindia viti 182, muungano wa siasa za wastani wa rais Macron ukipata viti 168 huku chama cha National Rally (RN) na washirika wake wamejikusanyia viti 143.
Hata hivyo hakuna muungano ulioweza kupata wingi wa viti bungeni, jambo linalotishia kuitumbukiza Ufaransa katika msukosuko wa kisiasa na kiuchumi.
Wafaransa wapiga kura duru ya pili ya uchaguzi wa Bunge
Muungano wa NFP umesema utatangaza jina la mgombea wa nafasi ya Waziri Mkuu.
"Kwa kuzingatia mantiki ya kitaasisi, ni juu yetu sasa kutafuta suluhu. Waziri Mkuu mzuri ni lazima aitulize nchi, na alete mshikamano ndani ya kundi lake," alisema Marine Tondelier Kiongozi wa chama cha kijani EELV kilicho sehemu ya muungano huo Marine Tondelier.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo Gabriel Attal, anayepanga kujiuzulu, amesema nchi yake inakabiliwa na hali ya kisiasa ambayo haijawahi kushuhudiwa.