Muuwaji wa watu 20 nae auwawa
9 Februari 2020Hatua hiyo inaufikisha kikomo mkwamo wa takribani masaa 17, ambao umesababisha pia idadi kubwa ya watu kujeruhiwa. Hata hivyo bado haijaweza kufahamika ni idadi gani hasa ya watu ambao imekwama katika upande wa 21 wa jengo lenye maduka mengi la Nakon Ratchasima. Eneo hilo ndilo ambalo, muuwaji alijificha baada ya kufanya tukio kwa kutumia silaha ambayo ameiiba katika kambi yake ya jeshi.
Namna muuwaji alivyouwawa
Kiongozi wa kukabiliana na vitendo vya uhalifu Jirabhob Bhjridej alisema, muuwaji ambae alifahamika kwa jina la Sajenti Meja Jakrapanth Thomma aliuawawa kwa kupigwa risasi mapema Asubuhi. Hatua hiyo inatokana na jitihada ya kukabiliana nae katika eneo la chini la jengo ambalo alikuwa kajificha kwa masaa kadhaa.
Kwa mujibu wa dokta wa hospitali inayotibu majeruhi kwa sasa ya Korat, Narinrat Pitchayakamin anasema taarifa rasmi zinaonresha idadi ya waliuwawa ni 20 na waliojeruhiwa 42. Lakini hata hivyo haijaweza kuwa wazi kama kuna waathirika wengine katika jengo hilo kubwa la maduka, ambalo lilikuwa na watu wengi ambao walifika kwa ajili ya kujipatia huduma zao kwa siku ya Jumamosi.
Polisi mmoja ni miongoni mwa waliouwawa katika operesheni ya kumtia nguvuni mwarifu na vilevile sehemu ya video yake ilisambazwa kupitia mtandao wa Facebook. Hata hivyo video hilo ilifutwa na shirika lenye kuratibu mwenendeo wa mtandao huo kwa madai kuwa ilikuwa inakiuka miika ya usambazaji. Na kutangaza kuwa inafuatilia kwa kina kuhakikisha kila taarifa itakayosambazwa kuhusu mkasa huo inadhibitiwa kimaadili.