1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvua inayonyesha Kenya huenda ikasababisha maafa makubwa

6 Mei 2020

Wataalamu wa jiolojia wanaeleza kuwa mvua kubwa inayonyesha nchini Kenya huenda ikafichua mipasuko ya ardhi huku matukio ya kukatika kwa baadhi ya barabara yakizidi kuripotiwa. Wakaazi huko wahofia usalama wao

Hawaii Vulkanausbruch
Picha: picture-alliance/AP Photo

Wakaazi wa Shaabab mtaa mmoja mjini Nakuru waliamkia taswira ya kipekee kuona barabara imepasuka karibu na makaazi yao, athari ya mvua kubwa iliyonyesha usiku kucha, nusra imuangamize dereva mmoja wa uchukuzi. Wanasema barabara hiyo ilikuwa imeanza kubonyea siku tatu kabla ya tukio hilo.

Hili sio tukio la kwanza kutokea eneo la bonde la ufa, kwani mwezi uliopita barabara ya eneo la Narok ilikatika mara mbili na kusitisha usafiri kutoka pande zote mbili.

Maeneo ya Subukia na Mau Narok pia yameshuhudia matukio ambapo ardhi inagawanyika kwenye nyumba au shambani na hata tukio ambapo bwawa liligawanyika na kuyameza maji yote.

Serikali imewahusisha wataalam kutoka kampuni za kuzalisha umeme za GDC (Andika kirefu chake badala ya kutumia kifupi chake) na KENGEN kutathmini chanzo cha mipasuko hiyo ya ardhi na kiasi ilichoenea.

Mvua kubwa inayonyesha inafichua mipasuko iliyo ardhini

Picha: picture-alliance/AP

Akizungumza na waandishi habari walipozuru barabara hiyo, Paul Ngugi mtaalam wa jiolojia kutoka kampuni ya GDC anaonya kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mvua kubwa inayonyesha inafichua mipasuko iliyo kwenye ardhi.

"Wakati mwingeni mvua inaponyesha mipasuko hii hujaa maji na kufunguka. Pia ikiwa imepata uzio mwingi, maji yanapoingia ndani kwa wingi yanailainisha na kuilegeza na hivyo kuiwezesha kusonga. Haya ni kulingana na uchunguzi wetu wa awali lakini timu yetu itakuwa ikifanya uchunguzi wa kitaalam pamoja na KENGEN. Kwa sasa tumeweza kutathmini kwamba huu ni mpasuko uliokuwepo awali”.

Wachambuzi wanayaona matukio haya kama dhihirisho kwamba sehemu ya ardhi iliko eneo la bonde la ufa sio imara na matukio kama haya huenda yakazidi kushuhudiwa.

Hata hivyo akisisitiza kwamba matukio haya hayana uhusiano wowote na shughuli ya uchimbaji mvuke inayoendeshwa katika eneo la bonde la ufa, Gavana wa kaunti ya Nakuru (taja jina) amesema wanatarajia ripoti kamili kutoka kwa wataalam katika muda wa wiki moja ambapo watashauri ni katika maeneo yapi watu watahitajika kuhama ili kuokoa maisha.

Mvua kubwa inayonyesha nchini Kenya inazidi kusababisha maafa, ikiripotiwa kuwa watu 30 wamekufa kutokana na mafuriko, ambayo sasa imefikia idadi ya watu 194 tangu mvua ianza. (hizi idadi za vifo vipi? mbona wasema 30 halafu 194? 30 ni wapi na 194 ni nchi nzima?

Chanzo: Wakio Mbogho, DW, Nakuru