1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Mvua kubwa na maporomoko yasababisha maafa Korea Kusini

15 Julai 2023

Watu 24 wamekufa na wengine kumi hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko Korea Kusini. Haya yamesemwa leo na maafisa nchini humo.

Südkorea Wetter l Überschwemmungen in Yecheon l Rettungsarbeiten
Picha: Yonhap/REUTERS

Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imesema kuwa vifo hivyo vilivyotokea jana, vilisababishwa na maporomoko ya ardhi na majengo kutokana na mvua hiyo. Wizara hiyo imeongeza kuwa watu wawili kati ya walioripotiwa kupotea, walisombwa na maji wakati mto mmoja ulipofurika katika jimbo la Kaskazini la Gyeongsang.

Zaidi ya wakazi 6,400 katika eneo la Goesan wameamriwa kuyahama makazi yao

Wizara hiyo imeendelea kusema kuwa zaidi ya wakazi 6,400 katika eneo la Goesan wameamriwa kuyahama makazi yao mapema leo wakati bwawa la Goesan lilipoanza kufurika kutokana na mvua hiyo na kuzamisha vijiji katika sehemu za bondeni zilizo karibu na eneo hilo. Waziri mkuu wa nchi hiyo Han Duck-soo amewahimiza maafisa kuchukuwa hatua za tahadhari dhidi ya mafuriko ya mito na maporomoko na kutoa ombi la msaada wa operesheni za uokoaji kutoka kwa wizara ya ulinzi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW