1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvua kubwa zasababisha daraja kuu Marsabit kuvunjika

2 Novemba 2023

Wakaazi katika eneo la Kargi jimboni Marsabit Kenya, wameandamana wakiomba kupelekewa chakula kwa helikopta kutokana na mvua kubwa zilizopelekea kuvunjika kwa daraja kuu linalounganisha eneo hilo.

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa Kaskazini mwa Kenya
Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa Kaskazini mwa Kenya Picha: picture alliance/Photoshot

Kwa siku ya tano idadi kubwa ya wakaazi hao hawajapata mlo huku watoto na akina mama wajawazito wakiathirika zaidi.
Kulingana na mzee Master Elei mmoja wa waandamanaji hao, serikali imewatelekeza.
 
Mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikali pamoja na serikali ya jimbo la Marsabit, kwa wakati huu yanaendelea kupeleka misaada kwa waathiriwa wa mafuriko katika eneo bunge la Laisamis.
 
Angalau familia mia mbili kutoka eneo la Logologo zimehamishwa kutokana na mafuriko.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW